Friday, November 14, 2014

Msalaba ni nini?


 Msalaba ni Upatanisho,Upendo na Ukombozi. Haya yote yamebebwa na mbeba Msalaba  Yesu Kristo Bwana WETU. Yesu ni kiungo mhimu kwa maisha ya kila mwanadamu kwani ndiye aliyejitoa kufanya tusogee miguuni pa Mungu kwani hatukustahili kwa kuwa tulitenda dhambi. Hivyo kwa kupigwa kwake tunasema tumepona,huruma ya Mungu kwa wanadamu ni kubwa sana kwani jehanamu haikuubwa kwa ajili ya Mwanadamu ni kwa ajili ya Shetani ila kwa kukosa kutii kwetu adhabu hii tnashiriki ila ukiamua kumpa maisha yako una kuwa huru na ghadhabu yake. Mungu kumtoa mwanae pekee ni kwa ajili yangu na yako hivyo tukubali kuifuata Neema hii.