Saturday, December 20, 2014

Mwimbaji Peter Haonga asema Waimbaji Binafsi tunakosa kuaminika kwa sababu ya kupenda hela.

 Peter Haonga ni mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania. Mpaka sasa ana album Moja ambayo ipo  tayari kwa mfumo wa Audio CD iitwayo Ee Nafsi Yangu, muda wowote itakuwa imekamilika video yake inayo fanywa na kampuni ya Mwamakula Production yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam. Album ya pili ipo kwenye maandalizi ya  kurekodiwa ambapo mpaka sasa tayari zipo nyimbo tatu, mojawapo wa hizo ni Nasikia Kuitwa.

Huduma hii ya uimbaji ni huduma kama zilizo huduma zingine inagawa kila mtu na uelewa wake ila  kuna haja kubwa jamii ielewe na kuheshimu huduma hii kama zilivyo huduma nyingine. Na siku zote adui namba moja ni wa nyumbani mwako, nasema hivi kwa sababu sisi wenyewe waimbaji kuna  kunadharauliana kulingana na majina kuna misemo mingi au Lugha zinazo tumika kuweza kuweka matabaka  kuna staa na underground ila tunashindwa kutambua kwamba staa wa kwanza ni Yesu sisi ni watenda kazi tu kwake. Wito  wangu kwa waimbaji wenzangu tushikamane.

 Katika kumtumikia Mungu kuna changamoto mbalimbali ya kwanza kwangu imekuwa changamoto kubwa ni kutukuamiwa kwa watu. Sababu kubwa ni kwamba waimbaji binafisi wanapenda sana hela kuliko utumishi. Unajua kila mtu na alivyoitwa na Mungu mimi si fanyi mziki kwa sababu ya kipato katika maisha yangu ni kwa ajili ya utumishi zaidi. Biblia ipo wazi kwa kila eneo anitumikiaye na kuniweka kuwa wa kwanza si mwacha hivyo naamini kwamba Bwana haweze kuniacha nikapungukiwa kamwe. Pili Waimbaji wakubwa kudharau waimbaji wadogo kama mnilivyo tangulia kusema hapo awali. Hii husababisha wengine kuacha huduma kabisa na huduma za watu wachanga kuwa duni. Tatu Ukosefu wa fedha pia ni tatizo inafanya mtu ushindwe kutimiza kusudi la Mungu kwa wakati huisika mziki wa Tanzani haukuwi kwa ukosefu wa fedha.