Thursday, January 1, 2015

Mwaka Mpya Ibada Leo

Nguzo nne za Kanisa ni Neno la Mungu, Imani, Utakatifu &Utii. kama kanisa likijengwa kwa msingi wa Neno la Mungu ambae ni Kichwa cha kanisa yaani Kristo Yesu basi kuzimu halitalivunja hilo kanisa .Tanzania niwakati sasa wa kulijenga kanisa kufuatia nguzo hizi Nne za kanisa.

Saturday, December 20, 2014

Mwimbaji Peter Haonga asema Waimbaji Binafsi tunakosa kuaminika kwa sababu ya kupenda hela.

 Peter Haonga ni mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania. Mpaka sasa ana album Moja ambayo ipo  tayari kwa mfumo wa Audio CD iitwayo Ee Nafsi Yangu, muda wowote itakuwa imekamilika video yake inayo fanywa na kampuni ya Mwamakula Production yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam. Album ya pili ipo kwenye maandalizi ya  kurekodiwa ambapo mpaka sasa tayari zipo nyimbo tatu, mojawapo wa hizo ni Nasikia Kuitwa.

Huduma hii ya uimbaji ni huduma kama zilizo huduma zingine inagawa kila mtu na uelewa wake ila  kuna haja kubwa jamii ielewe na kuheshimu huduma hii kama zilivyo huduma nyingine. Na siku zote adui namba moja ni wa nyumbani mwako, nasema hivi kwa sababu sisi wenyewe waimbaji kuna  kunadharauliana kulingana na majina kuna misemo mingi au Lugha zinazo tumika kuweza kuweka matabaka  kuna staa na underground ila tunashindwa kutambua kwamba staa wa kwanza ni Yesu sisi ni watenda kazi tu kwake. Wito  wangu kwa waimbaji wenzangu tushikamane.

 Katika kumtumikia Mungu kuna changamoto mbalimbali ya kwanza kwangu imekuwa changamoto kubwa ni kutukuamiwa kwa watu. Sababu kubwa ni kwamba waimbaji binafisi wanapenda sana hela kuliko utumishi. Unajua kila mtu na alivyoitwa na Mungu mimi si fanyi mziki kwa sababu ya kipato katika maisha yangu ni kwa ajili ya utumishi zaidi. Biblia ipo wazi kwa kila eneo anitumikiaye na kuniweka kuwa wa kwanza si mwacha hivyo naamini kwamba Bwana haweze kuniacha nikapungukiwa kamwe. Pili Waimbaji wakubwa kudharau waimbaji wadogo kama mnilivyo tangulia kusema hapo awali. Hii husababisha wengine kuacha huduma kabisa na huduma za watu wachanga kuwa duni. Tatu Ukosefu wa fedha pia ni tatizo inafanya mtu ushindwe kutimiza kusudi la Mungu kwa wakati huisika mziki wa Tanzani haukuwi kwa ukosefu wa fedha.

Thursday, December 18, 2014

Reform Evangelical Singers Choir- Ikiwa Watu Wangu oficial video Msalaba...

Hatimaye kwaya ya Reform Evangelical Singers Wakamilisha uandaaji wa album yao ya Tatu iitwayo PIGANA NAO. Ambayo imefanya na Msalaba MEDIA chini ya Mwongozaji Abson Mhanje. Muda si mrefu itapatikana madukani kote usikiose kuipata nakala halisi na Mungu wa mbinguni atakubariki kwa kujitoa kwako  kwa ajilim ya injili .



Hakika ni furaha tupu kumtumikia Mungu.Kazi ya Bwana haina majuto kamwe ukipata nafasi ya kutumika ikiwa babo kija na shukru Mungu kwani wengi hawakupata Neema hiyo.

Nico Amani Mwakyeja





Hi hapa Vid

Mary Goreth mbioni kukamilisha Maandalizi ya video




Wednesday, December 17, 2014

TB Joshua at Colombia 07.27.14

Faida kubwa kuliko zote kwaa Nchi yeyote ile ni kumheshimu Mungu. Nchini Colombia kuna dini nyingi tofauti tofauti lakini wanamheshimu Mungu na kuelewa kazi na matendo yake makuu. Swali langu  Tanzani lini roho hii ya kumtanguliza Mungu itaingia kwa taifa. Mungu tusaidie kama Taifa tutambue matendo yako makuu kama Taifa na si mtu binafsi