Tuesday, February 23, 2016

Nabii Okoa Gamba

 Picha kumi na mbili za Nabii Okoa Gamba. Nabii okoa Gamba ni mtumishi ambaye Mungu anamtumia kwa kizazi hiki kipya kwa maana anachimbua siri za shetani anavyo waonea watu kwa kuwafunga na vifungo vya kila aina.Hakika Mungu anajitukuza mahali pale pa hema la Kanisa la Wafalme Kituo Cha Sauti ya Unabii,Tabata Bima.
 Unafikaje Kanisa la Wafalme- Popote ulipo panda gari za Tabata iwe za Kimanga/Segerea&Kinyerezi shuka kituo Tabata Bima Uliza mtaa wa Tenge nyuma ya ofisi za serikali za mitaa utakuwa umefika.

 Hapa Nabii akihubiri na kutabiri ibadani


 Mchungaji Msaidizi Ester akipokea baraka kutoka kwa Nabii
 Mama huyu akishuhudia kile mungu amefanya baada ya kutopata mtoto kwa miaka kumi na  tatu (13) kwa MAOMBI ya Mtumishi wa Mungu Gamba amemzaa mtoto huyu ingawa madakitari walisema anatatizo kizazi chake kimelegea
 Kijana HUYO kila kiungo ndani ya mwili wake kulikuwa kimehalibika kutokana na mateso ya shetani. maini yalioza, Figo zilishindwa kufanya kazi amelala hospitari kipindi cha mwaka mmoja hakupata uponyaji wakamwandikia kwenda India ila hakwenda kwanio alipata neema ya kufika ibadani na Mungu akamponya

 Je shida yako ni nini? futa machozi,usilie BWANA ameona kilio chako mbebeshe yeye fadhaa zako, umechosha na umasikini,umesahaulika,umekataliwa,unaupweke, Njaa, yatima, magonjwa,umeachwa na mmeo au mkeo? Fika NYUMBANI MWA BWANA nawe utapumzishwa kwa hakia Amina ubarikiwe na karibu sana.

Wednesday, January 6, 2016



Msalaba MEDIA ni kampuni ya kizalendo nchini Tanzania tupo tayari kuwahudumia wanamuziki wa kila kiwango kwa ubora atakao. Njoo tuzungumze, tufanye,uridhike na ufaidike. 

Tuesday, September 15, 2015

Rejoice Choir TAG Shinyanga

Ile choir maalufa katika mji wa Shinyanga imekamilisha kurekodi video yao toleo la pili liitwalo Watumishi. Katika hatua za awali kabisa kazi hii imeenda sasa na mipango endelevu ya kwaya hiyo ktk kumtumikia Mungu kwa  njia ya uimbaji. Kwa upande wa kampuni iliyohusika kurekodi ambayo ni Msalaba MEDIA  walipohojiwa na www.absonmhanje.blogspot.com wamesema maandalizi ya ya kurekodi  albumu hiyo mhimu yalikuwa sawa hivyo wadau na wapenzi wa muziki wa injili Tanzani wategemee kupata video yenye ubora wa hali ya juu. Kwani wanasema Msalaba MEDIA daima ni Standard Quality Excellence hawakuishia hapo nwakasema kazi uliyoiona jana ni tofauti na ya kesho kwani wanaamini katika Forward We Go

Tuesday, June 16, 2015

Safina Choir Arusha

Ni Ebenezer hakika hatimaye kwaya iliyokuwa na maono ya mda mrefu kabisa jijini Arusha imekamilisha kurekodi video ya album iitwayo FUNUA











Thursday, January 1, 2015

Mwaka Mpya Ibada Leo

Nguzo nne za Kanisa ni Neno la Mungu, Imani, Utakatifu &Utii. kama kanisa likijengwa kwa msingi wa Neno la Mungu ambae ni Kichwa cha kanisa yaani Kristo Yesu basi kuzimu halitalivunja hilo kanisa .Tanzania niwakati sasa wa kulijenga kanisa kufuatia nguzo hizi Nne za kanisa.

Saturday, December 20, 2014

Mwimbaji Peter Haonga asema Waimbaji Binafsi tunakosa kuaminika kwa sababu ya kupenda hela.

 Peter Haonga ni mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania. Mpaka sasa ana album Moja ambayo ipo  tayari kwa mfumo wa Audio CD iitwayo Ee Nafsi Yangu, muda wowote itakuwa imekamilika video yake inayo fanywa na kampuni ya Mwamakula Production yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam. Album ya pili ipo kwenye maandalizi ya  kurekodiwa ambapo mpaka sasa tayari zipo nyimbo tatu, mojawapo wa hizo ni Nasikia Kuitwa.

Huduma hii ya uimbaji ni huduma kama zilizo huduma zingine inagawa kila mtu na uelewa wake ila  kuna haja kubwa jamii ielewe na kuheshimu huduma hii kama zilivyo huduma nyingine. Na siku zote adui namba moja ni wa nyumbani mwako, nasema hivi kwa sababu sisi wenyewe waimbaji kuna  kunadharauliana kulingana na majina kuna misemo mingi au Lugha zinazo tumika kuweza kuweka matabaka  kuna staa na underground ila tunashindwa kutambua kwamba staa wa kwanza ni Yesu sisi ni watenda kazi tu kwake. Wito  wangu kwa waimbaji wenzangu tushikamane.

 Katika kumtumikia Mungu kuna changamoto mbalimbali ya kwanza kwangu imekuwa changamoto kubwa ni kutukuamiwa kwa watu. Sababu kubwa ni kwamba waimbaji binafisi wanapenda sana hela kuliko utumishi. Unajua kila mtu na alivyoitwa na Mungu mimi si fanyi mziki kwa sababu ya kipato katika maisha yangu ni kwa ajili ya utumishi zaidi. Biblia ipo wazi kwa kila eneo anitumikiaye na kuniweka kuwa wa kwanza si mwacha hivyo naamini kwamba Bwana haweze kuniacha nikapungukiwa kamwe. Pili Waimbaji wakubwa kudharau waimbaji wadogo kama mnilivyo tangulia kusema hapo awali. Hii husababisha wengine kuacha huduma kabisa na huduma za watu wachanga kuwa duni. Tatu Ukosefu wa fedha pia ni tatizo inafanya mtu ushindwe kutimiza kusudi la Mungu kwa wakati huisika mziki wa Tanzani haukuwi kwa ukosefu wa fedha.

Thursday, December 18, 2014

Reform Evangelical Singers Choir- Ikiwa Watu Wangu oficial video Msalaba...

Hatimaye kwaya ya Reform Evangelical Singers Wakamilisha uandaaji wa album yao ya Tatu iitwayo PIGANA NAO. Ambayo imefanya na Msalaba MEDIA chini ya Mwongozaji Abson Mhanje. Muda si mrefu itapatikana madukani kote usikiose kuipata nakala halisi na Mungu wa mbinguni atakubariki kwa kujitoa kwako  kwa ajilim ya injili .



Hakika ni furaha tupu kumtumikia Mungu.Kazi ya Bwana haina majuto kamwe ukipata nafasi ya kutumika ikiwa babo kija na shukru Mungu kwani wengi hawakupata Neema hiyo.

Nico Amani Mwakyeja





Hi hapa Vid